Programu inayolenga kwa ujumla Waislamu wanaotaka kupokea elimu ya kisheria ya lazima, (yanayojulikana katika dini kwa lazima, nayo ni yale ambayo haimpasi Muislamu kutoyajua), kwa Mapokezi (Sanad) yenye kuungana, ambapo programu hii inajumuisha idadi ya masomo yanayowasilishwa kwa mujibu wa mpangilio wa kielimu uliomzuri na kwa njia rahisi na nyepesi, na masomo yake yapo wazi na hayajafungwa kwa muda maalumu, Mwanafunzi anaweza kupitia humo kujisajili na kusoma masomo na kuyakamilisha katika wakati na muda unaomfaa yeye.