Ni programu ya elimu iliyoandaliwa kwa misingi iliyo thabiti, inayojumuisha ngazi na hatua kadhaa za masomo. Inalenga kumlea na kumwandaa mwanafunzi mwenye ujuzi madhubuti katika elimu za Shariah na nyenzo zake. Programu hii imekusudiwa kwa wale wenye nia na uwezo wa kujitolea katika nyakati maalumu zilizopangwa.
Masomo yanafanyika ndani ya muda uliopangwa kulingana na ratiba ya kila somo (kozi), na yanajumuisha vikao vya moja kwa moja na walimu, dirisha la mijadala, shughuli mbali mbali na baadhi ya kazi za mwanafunzi, pamoja na mfumo makini wa mitihani. Mwanafunzi anatakiwa kufuatilia masomo na kuwasilisha kazi zinazohitajika kulingana na ratiba iliyoandaliwa.