Chuo cha Elimu cha Sanad ni lango la kielimu la kidijitali la DarulMustafa mjini Tarim kwa masomo ya Kiislamu. Hutoa mtaala wa kati na kati wa kielimu, kimalezi na kulingania kutoka DarulMustafa ya Tarim, kwa mtazamo unaounganisha uhalisia wa kuipokea elimu kwa mapokezi sahihi na kuendana na zama za kidijitali.
Chuo hiki kinasimama juu ya uaminifu wa kielimu ulio imara, unaopata nguvu kutokana na mapokezi sahihi yenye kuendelea bila kukatika; ambapo elimu za Sharia Tukufu na fani zake hupokelewa kutoka kwa Mashekhe na Walimu waliopokea elimu yao kutoka kwa Wanazuoni wakubwa waliothibiti katika elimu kwa mapokezi yaliounganika na kuendelea hadi kwa Mtume wetu Muhammad rehema na amani ziwe juu yake pamoja na Aali zake na Masahaba zake.
Kupitia programu za kielimu zilizo na ngazi mbalimbali zinazochanganya elimu, mwenendo mzuri na kulingania, Chuo cha Sanad humuwezesha mwanafunzi popote alipo duniani kuunganishwa na urithi wa elimu ya Mtume, na kupokea mtaala wa kielimu, kimalezi na kulingania wa DarulMustafa ya Tarim kwa mtindo wa kisasa na kitaalama unaokuza maarifa, kuitakasa nafsi na kuitumikia dini na Umma
Ili kuchangia katika kuitumikia Sharia Tukufu, na kutekeleza wajibu wa kueneza urithi mtukufu wa Unabii, ambao hauwezi kuhifadhiwa wala kutekelezwa ipasavyo isipokuwa kupitia watu waliobobea na kuhitimu kwa ajili yake. Hili hufanyika kupitia: (kuimarisha urithi wa Kinabii ndani ya nafsi zitakazoyaeneza).
Kufikia kuongoza katika nyanja ya elimu ya kielektroniki yenye malengo ya kheri, na kiwe Chuo cha Sanad chaguo la kwanza kwa wanaotamani kupokea elimu yenye mapokezi ya kati na kati kwa Ahli -Sunna wal-Jamaa (mtaala wa kielimu, kimaadili na kulingania wa DarulMustafa ya Tarim kwa masomo ya Kiislamu).
- Kufundisha elimu za Sharia kwa mapokezi yaliyoungana kwa usahihi na kwa njia ya urithi wa kielimu, sambamba na kutumia mbinu na njia za kisasa zenye manufaa na kuunganisha elimu na uhalisia ili kurahisisha utekelezaji.
- Kuzitakasa nafsi kwa ikhlasi ya nia, kuitakasa mioyo na kuendeleza maadili mema.
- Kukuza ndani ya nyoyo utukufu wa kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kutekeleza wajibu wake, pamoja na kuimarisha uwezo na juhudi katika maelezo mazuri na kufikisha kheri kwa wigo mpana iwezekanavyo.
- Kunufaika na njia za kisasa katika kurahisisha kupokea elimu kutoka kwa wanazuoni na kuhifadhi urithi wao wa kielimu, pamoja na kupokea mtaala wa Dar al-Mustafa – Tarim kwa masomo ya Kiislamu kwa wale wasioweza kufika chuoni au kujitolea kikamilifu kwa masomo, yote hayo kwa mujibu wa maono na mbinu ya kielimu iliyo wazi.