Chuo cha Sanad kimempokea Shekhe Auzair Khilwati, Mwalimu katika Taasisi ya Maqasid Nchini Marekani, Katika ziara hiyo alijifunza mengi kuhusu Dira ya Chuo hicho, pamoja na programu zake za Elimu ya Sharia zenye misingi imara, zinazosomeshwa kwa njia ya mitandao bila malipo; kwa lengo la kuifikisha Elimu ya Sharia iliyosahihi kwa Waislamu katika maeneo mbalimbali ya Ulimwengu.
Katika ziara hiyo, Shekhe alipata fursa ya kufahamu mfumo wa kielimu unaofuatwa na Chuo, maudhui zinavyowasilishwa, ubora wa jukwaa la masomo, pamoja na programu na Kozi zinazotolewa. Alieleza kuvutiwa sana na wazo la kuanzishwa kwa Chuo hicho, akisisitiza kuwa ni Chuo cha kielimu cha kipekee, na kwamba kuna haja kubwa sana ya Vyuo vya aina hii katika Nchi za Magharibi, hasa kwa kuwa Chuo kinakusanya misingi madhubuti ya Elimu, umahiri katika uwasilishaji, na upatikanaji wa masomo bila malipo- Mambo ambayo ni mara chache sana kupatikana yote kwa pamoja katika Chuo cha kielimu kwa kiwango hiki.
Pia katika kikao hicho yalifanyika majadiliano yenye manufaa kuhusu fursa za ushirikiano wa pamoja, kwa lengo la kufikisha ujumbe wa Chuo kwa Waislamu Nchini Marekani na katika Nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza. Sambamba na hilo ilijadiliwa namna ya kuunga mkono na kueneza shughuli za Chuo katika Jamii hizo, pamoja na kufanya usajili wa baadhi ya Kozi za kielimu kwa lugha ya Kiingereza, ili ziwe karibu zaidi na ziwafikie wanafunzi wengi wa Elimu katika Nchi za Magharibi.
Ziara hii ni sehemu ya juhudi za Chuo cha Sanad za kujenga ushirikiano wa kimataifa katika nyanja za Elimu, kuimarisha uwepo wake ili kutimiza lengo lake la kueneza Elimu ya Sharia kwa njia sahihi na kuifikisha kwa kila Muislamu popote alipo, kwa lugha yake, na kwa viwango vya juu vya kielimu na kiufundishaji.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu azibariki juhudi hizi, azijalie zikubalike, na azifanye kuwa hatua yenye baraka katika kuitumikia Elimu na watu wake katika maeneo mbalimbali ya Ulimwengu.