▪️ Chuo cha Sanad cha Elimu za Sharia kilipokea kikundi cha wageni wa kielimu katika washiriki wa Kongamano la Walinganiaji ambalo lilifanyika DarulMustafa ya Tarim kwa Masomo ya Kiislamu. Katika kikundi cha wageni hao alikuwemo Shekhe Walid Faraj Atwiyyah, Mwanzilishi wa Chuo cha Zaytun cha Kufufua Urithi wa Elimu kutoka Jamhuri ya Tunisia, pamoja na Doctor Shekhe Muhammad Yasir Qadhman. Katika ziara hiyo, wageni hao walifahamishwa kuhusu dira na malengo ya Chuo cha Sanad na wakajionea jukwaa lake la Elimu kwa njia ya mtandao pamoja na programu zake za kielimu na malezi, zinazolenga kueneza elimu sahihi ya Kiislamu kwa mujibu wa mfumo wa kielimu wa Chuo cha DarulMustafa cha Masomo ya Kiislamu huko Tarim, na kuifikisha Elimu hiyo kwa Waislamu duniani kote kwa lugha mbalimbali.
▪️ Ziara hiyo ilijumuisha kikao kilichojadili njia za ushirikiano na ukamilishaji wa juhudi baina ya pande mbili, pamoja na kutafiti maeneo yanayowezekana kuchangia na kuwezesha kazi ya Kulingania, kueneza Elimu ya Sharia, kuimarisha juhudi za pamoja katika kueneza elimu yenye manufaa, na kunufaika na uwezo na uzoefu wa pande zote mbili ili kufanikisha malengo ya pamoja.
▪️ Ziara hii imekuja katika mwelekeo wa Chuo cha Sanad wa kujenga ushirikiano madhubuti na taasisi pamoja na vyombo vya Kielimu na Kulingania, kwa lengo la kupanua wigo na athari zake, kuimarisha ujumbe wa kueneza elimu sahihi ya Kiislamu, na kueneza Elimu kwa mbinu za kisasa na kwa lugha mbalimbali.