Chuo cha Sanad kilimpokea Mheshimiwa Shekhe Sameer Zulfikar, Mudir wa Maahad Juneyd Islamy ya Zanzibar, ambaye pia ni mmoja wa walimu wa Chuo katika lugha ya Kiswahili, katika mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya kujadili njia za kuendeleza masomo ya Chuo kwa upande wa Lugha ya Kiswahili na kuimarisha kuenea kwake kwa watu wanaozungumza lugha hiyo katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki.
Mkutano huo ulijadili mawazo na mipango kadhaa itakayochangia kuinua maudhui ya kielimu yanayotolewa kwa lugha ya Kiswahili, kwa namna itakayotekeleza ujumbe wa Chuo wa kufikisha Elimu za Sharia zilizo sahihi kwa idadi kubwa zaidi ya Waislamu kwa lugha zao mbalimbali.
Pia pande hizo mbili zilijadili uwezekano wa kutekeleza Kozi kadhaa za kielimu kwa lugha ya Kiswahili, pamoja na kuimarisha nyanja za ushirikiano kwa yale yatakayo wezesha kueneza Elimu ya Sharia na kupanua wigo wa kunufaika na Programu za Chuo katika jamii zinazozungumza Kiswahili.
Ziara hii inatokana na juhudi za Chuo cha Sanad za kuendeleza majukwaa yake ya lugha mbalimbali na kupanua uwepo wake Duniani kutokana na ujumbe wake wa kutoa Elimu za Sharia zilizo sahihi kwa mujibu wa mbinu madhubuti za kielimu, na kupatikana bila malipo kwa wanaojifunza kote Duniani kwa lugha zao mbalimbali.